NAFASI ZA KAZI ZA MUDA TUME YA UCHAGUZI TANZANIA
1. Msimamizi wa Uchaguzi (Nafasi moja)
Majukumu
(i) Kuratibu na kusimamia shughuli za Uchaguzi katika Wilaya yake.
(ii) Kusimamia na kufuatilia utendaji kazi wa Watendaji wa Uchaguzi walio chini yake.
(iii) Kutunza vifaa vya Uchaguzi katika Wilaya husika.
(iv) Kusimamia matumizi ya fedha za Uchaguzi.
(v) Kushirikiana na kushauriana na Mratibu wa Uchaguzi katika kuleta ufanisi kwenye shughuli za Uchaguzi.
(vi) Kutoa taarifa ya mwenendo wa hatua za uchaguzi kwa kuzingatia maelekezo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi
2.Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Ngazi ya Jimbo (Nafasi mbili) Majukumu
(i) Kuwa kiungo kati ya Jimbo na Wilaya.
(ii) Kusimamia shughuli zote za Uchaguzi katika Jimbo husika.
(iii) Kumsaidia Msimamizi wa Uchaguzi katika masuala yote ya Uchaguzi.
Ni nzuri hii
ReplyDelete